-
Kiswahili Kitukuzwe Kidato Cha 2
Hili ni toleo jipya la Kiswahili kwa Kidato cha Pili, Kitabu cha Wanafunzi. Kitabu hiki ni cha pili katika mfululizo wa vitabu vinne vya Kiswahili kwa shule za upili. Kitabu hiki kimefuata mfumo wa elimu wa 8-4-4 na kufanyiwa marudio kulingana na silabasi mpya ya Kiswahili ya Kidato cha Pili. Katika toleo hili, maelezo zaidi juu ya nyanja mbalimbali za lugha yameshughulikiwa kama vile, mpangilio mpya wa ngeli, kusoma kwa kina, na msamiati na istilahi kimuktadha. Pia, maswala ibuka kama vile maadili, UKIMWI na mazingira yamejitokeza. Mifano zaidi, michoro na picha zimetumiwa ili kufanya somo hili liwe la kuvutia.
-
Kiswahili Kitukuzwe Kidato Cha 3
Hili ni toleo la nne la Kiswahili kwa Kidato cha Tatu, Kitabu cha Wanafunzi. Kitabu hiki ni cha tatu katika mfululizo wa vitabu vinne vya Kiswahili kwa shule za upili.
Kitabu hiki kimefuata mfumo wa elimu wa 8-4-4 na kufanyiwa marudio kulingana na silabasi mpya ya Kiswahili ya Kidato cha Tatu
-
Kiswahili Kitukuzwe Kidato Cha 3 Kitabu Cha Mwalimu by Watuha
by Watuha
Hili ni toleo la nne la Kiswahili kwa Kidato cha Tatu, Mwongozo wa Walimu. Kitabu hiki ni cha tatu katika mfululizo wa vitabu vinne vya Kiswahili kwa shule za upili. Kitabu hiki kimefuata mfumo wa elimu wa 8-4-4 na kufanyiwa marudio kulingana na silabasi mpya ya Kiswahili kwa Kidato cha Tatu. Katika toleo hill, maelezo zaidi juu ya nyanja mbalimbali za lugha yameshughulikiwa kama vile, mpangilio mpya wa ngeli, kusoma kwa kina, na msamiati na istilahi kimuktadha. Pia, masuala ibuka kama vile maadili, UKIMWI na mazingira yamejitokeza. Mifano zaidi, michoro na picha zimetumiwa ili kufanya somo hili liwe la kuvutia. Ni kitabu ambacho walimu watafurahia kukitumia. -
Kiswahili kwa darasa la 8
Hili ni toleo la pili la Kiswahili kwa Darasa la Nane. Kitabu hiki. cha wanafunzi ni cha nane katika mfululizo wa vitabu vinane vya lugha ya Kiswahili kwa shule za msingi. Kitabu hiki kimezingatia kwa kina na kwa namna ya kipekee mada zote zilizomo katika silabasi ya Kiswahili ya 2002 kwa Darasa la Nane. Katika toleo hili, masuala nyeti yameshughulikiwa kwa uketo na usasa kama vile utaratibu wa ngeli kwa kuzingatia upatanisho wa viambishi kisarufi. Masuala ibuka kama vile haki za watoto, mazingira, UKIMWI, uadilifu, jinsia, ajira za watoto na afya yameshughulikiwa kwa upana na utaalamu wa kupigiwa mfano. Mifano, michoro ya rangi na picha nyingi zimetumiwa ili kulifanya somo hili liwe la kuvutia zaidi. Mazoezi kemkem yanayozingatia vipengele vyote katika silabasi yamejumuishwa ili kumhusisha mwanafunzi kikamilifu. Kitabu hiki kinawalenga wanafunzi kutoka mazingira na jamii mbalimbali. Vilevile kitabu hiki kina mitihani ya majaribio ili kumwandaa mwanafunzi ipasavyo kwa mtihani wa K.C.P.E.
-
Kiswahili Kwa Darasa la 8 Kitabu Cha Mwalimu by Watuha
by Watuha
Hii ni seti ya vitabu iliyojikita kwenye silabasi mpya ya shule za msingi na kunuiwa kuwasaidia wanafunzi kuongeza ujuzi wao wa lugha ya Kiswahili. Kila kitabu ni zao la utafiti wa kina wa mahitaji ya wanafunzi wa Kiswahili na kinakidhi matakwa yote ya lugha kwa kiwango husika. -
Kiswahili Mufti Darasa la 8 by Wallah
by Wallah
Toleo hili la Kiswahili Mufti 8 linatimiza kikamilifu mahitaji na mada zote za silabasi mpya iliyoanza kutekelezwa shuleni kuanzia 2003. Kitabu hiki kimeandikwa kwa uangalifu mkubwa ili kiweze kueleweka vizuri zaidi na wanafunzi wote kutoka mazingira mbalimbali. Msamiati uliotumika katika vifungu vya ufahamu unaafikiana vyema zaidi na uwezo wa lugha wa wanafunzi katika kiwango hiki. Toleo hili limeshughulikia kikamilifu maswala ibuka kama vile teknolojia ya habari na mawasiliano, katiba, rajua ya 2030, ufisadi na athari zake mbaya, mazingira, haki za watoto, UKIMWI, jinsia na maadili. -
Kiswahili Mufti Kioo cha Mtihani Mwongozo wa Mwalimu by Joseph Mwamburi, Wallah …
by Joseph Mwamburi, Wallah Bin Wallah
Kiswahili Mufti 8: Mwongozo we Mwalimu unampa mwalimu maelezo kamili kuhusiana na mbinu mwafakaza kutayarisha, kuendesha na kutathmini vipindi vya Kiswahili darasani. Mwongozo huu mpana sana unampa mwalimu maelekezo mwafaka yatakayomwezesha kuviandaa na kuviendesha vizuri vipindi vinavyoshughulikia vipengele vifuatavyo:
Mwongozo huu una mifano mwafaka ya maazimio ya kazi na ratilp ya vipindi itakayomwongoza mwalimu kuzingatia mbinu zifaazo za kutekeleza malengo yote ya somo. Pia, una majibu ya maswali yote yaliyomo kwenye kitabu cha wanafunzi. -
kiswahili sahili gd4 approved
Kiswahili Sahili, Gredi ya 4, ni kitabu kinachompa mwanafunzi fursa nzuri kutangamana na Mtaala wa Kiumilisi kupitia
mada na shughuli alizoandaliwa. Lengo hasa la mtaala huu mpya ni kumwezesha mwanafunzi kupata maarifa pamoja na kumjengea
umilisi mzuri wa masuala na maaarifa mbalimbali ili aweze kuyatumia katika maisha yake ya kila siku.
Kitabu hiki kinampa mwanafunzi nafasi ya kujenga umilisi wake katika lugha ya Kiswahili kupitia stadi zilizoshughulikiwa
humu.Kitabu hiki kinashughulikia kusikiliza na kuzungumza kwa namna inayomwezesha mwanafunzi wa Gredi ya 4 kujenga
matamshi, kutumia lugha vizuri kulingana na muktadha. Sehemu ya kusoma inampa mwanafunzi mbinu za kusoma kwa ufahamu,
kusoma kwa kina na kusoma kwa mapana na hivyo kumwezesha kujenga ufasaha wake, wa lugha. Kitabu hiki kinaangazia
stadi ya kuandika ambapo mwanafunzi anaongozwa hatua kwa hatua jinsi ya kuandika tungo za namna mbalimbali.
Sehemu ya sarufi inampa mwanafunzi fursa ya kujenga umahiri wake wa kutumia lugha kwa ufasaha. -
Kiswahili Sanifu Darasa la 8 by Bakhressa
by Bakhressa
Kiswahili Sanifu (toleo jipya) ni kozi inayotokana na utafiti wa kina kuhusu mahitaji ya wanafunzi wa shule za msingi katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Kozi hii itawawezesha wanafunzi kuinua viwango vyao vya msamiati. Pia itawapa fursa ya kupata na kutumia katika maisha yao maarifa mbalimbali watakayojifunza. Isitoshe, kozi hii itawapa nafasi ya kusoma kwa matengo anuwai na kujieleza kikamilifu wakitumia lugha ya Kiswahili sanifu. -
Kitabu changu cha Kiswahili by Njoroge
by Njoroge
Kitabu hiki kimeandikwa nu mwandishi mwenye tajriba pana ya kufundishc katika Shule za Chekechea nchini Kenya. Muundo wa kitabu hiki utamsaidia mwanafunzi kupata msingi imam wa elimu ya kiwango cha Chekechea. Mwanafunzi anahakikishiwa stadi muhimu zinazohitajika katika kujenga msingi dhabiti masomoni. Kitabu hiki kitamsaidia mwanafunzi:
Shop By Categories
- International Curriculum
- Marketplace – Used Books!
- National Curriculum
- TVET/Higher Learning
- Lab Equipment
- General Books
- International Curriculum
- Marketplace – Used Books!
- National Curriculum
- TVET/Higher Learning
- Lab Equipment
- General Books











