Access Kiswahili Sahili GD4 (Approved)
KShs600.00
Kiswahili Sahili, Gredi ya 4, ni kitabu kinachompa mwanafunzi fursa nzuri kutangamana na Mtaala wa Kiumilisi kupitia
mada na shughuli alizoandaliwa. Lengo hasa la mtaala huu mpya ni kumwezesha mwanafunzi kupata maarifa pamoja na kumjengea
umilisi mzuri wa masuala na maaarifa mbalimbali ili aweze kuyatumia katika maisha yake ya kila siku.
Kitabu hiki kinampa mwanafunzi nafasi ya kujenga umilisi wake katika lugha ya Kiswahili kupitia stadi zilizoshughulikiwa
humu.Kitabu hiki kinashughulikia kusikiliza na kuzungumza kwa namna inayomwezesha mwanafunzi wa Gredi ya 4 kujenga
matamshi, kutumia lugha vizuri kulingana na muktadha. Sehemu ya kusoma inampa mwanafunzi mbinu za kusoma kwa ufahamu,
kusoma kwa kina na kusoma kwa mapana na hivyo kumwezesha kujenga ufasaha wake, wa lugha. Kitabu hiki kinaangazia
stadi ya kuandika ambapo mwanafunzi anaongozwa hatua kwa hatua jinsi ya kuandika tungo za namna mbalimbali.
Sehemu ya sarufi inampa mwanafunzi fursa ya kujenga umahiri wake wa kutumia lugha kwa ufasaha.
Reviews
There are no reviews yet.