-
Insha Mufti Kioo cha Mwanafunzi by Wallah
Kioo Cha Mwanafunzi
Ufasaha Kamili Ngeli Sahihi Maendelezo Sahihi Msamiati Mwafaka Viambajengo Adhimu Misemo Aali: Tashdidi, Tanakali. Tanakani, Tashbihi, Methali, Nahau n.k. -
Common Mistakes in English by Fitikides
by Fitikides
Common Mistakes in English takes more than 550 examples of typical errors (for example, words that are often confused, misused, or used with the wrong preposition) and offers a correct version and explanation that will help students avoid making the same mistakes themselves. An invaluable book for students who are keen to ‘get it right’ every time. * Offers correct versions and explanations for more than 550 typical errors * Completely updated to reflect modern English usage -
Tenzi Tatu za Kale by MM Mulokozi
by MM Mulokozi
Kitabu hiki ni mkusanyo wa tenzi tatu za kale maarufu: Fumo Liyongo, uliotungwa na Muhamadi Kijumwa; Al Inkishafi, uliotungwa na Sayyid Abdalla bin Ali; na Mwanakupona, uliotungwa na Mwana Kupona binti Mshamu. Kitabu kimehaririwa na M.M. Mulokozi, profesa mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kilichapishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili mwaka 1999.Hizi ni kati ya tenzi maarufu kabisa katika ki-Swahili. Kwa msingi wa sanaa na maudhui, tenzi hizi zina hadhi kamili ya kuwemo katika orodha ambayo kwa ki-Ingereza huitwa “classics.”Fumo Liyongo ni hadithi inayomhusu shujaa Fumo Liongo, ambaye mimi, kutokana na utafiti wangu wa miaka mingi, napendelea kumwita Liongo Fumo. Huyu ni shujaa wa kale, labda miaka elfu moja iliyopita, na ndiye anayesifika kuliko wote tangu zamani katika jamii ya wa-Swahili.Alikuwa pandikizi la mtu, mwenye vipaji kadhaa: kuwashinda maadui, shabaha katika kutumia upinde na mshale, ufundi wa kutunga nyimbo na mashairi. Juu ya yote, alikuwa muungwana sana, mfano wa kuigwa. Lakini alifanyiwa visa na ndugu yake ambaye alikuwa mfalme, hadi hatimaye akauawa na kijana mdogo, ambaye alikuwa mpwa wake.Al Inkishafi ni utenzi wa tafakuri na falsafa kuhusu maisha, ambao umejikita katika kuuliza maana ya maisha ni nini. Mtunzi alilishughulikia suali hili kwa kuzingatia jinsi ustawi na utukufu wa wa-Swahili, hasa wa mji wa Pate, ulivyoanguka. Pate ulikuwa mji maarufu, wenye hadhi na mali, lakini kutokana na masaibu mbali mbali, ullipoteza hadhi hiyo na kuishia kuwa magofu.Hii dhamira imeshughulikiwa tangu zamani na waandishi wengi wa pande za Arabuni, Uajemi, Ulaya na sehemu zingine duniani. Wanafalsafa pia wamehoji maana ya maisha, hasa wanafalsafa wa mkondo wa “existentialism.”Mwana Kupona ni utenzi uliotungwa na mama kumuusia binti yake kuhusu maisha ya ndoa, wajibu wake katika maisha hayo, na wajibu wake kwa watu kwa ujumla. Huu ni utenzi maarufu sana, ambao ni chimbuko la tungo za waandishi wengine, kama vile Shaaban Robert. -
Kamusi Rasmi ya Picha by Yahya Mutuku
by Yahya Mutuku
Kamusi rasmi ya picha imeandikwa kwa upekee usiodhihirika katika kamusi nyingine. Kamusi hii ina sifa zifuatazo- Imeepuka mpangilio wa kialfabeti uliotumiwa na kamusi nyingine. Msamiati umepangwa kwa makundi badala ya kialfabeti kwa sababu wanafunzi katika kiwango hiki bado hawawezi kusaka msamiati kialfabeti (kiabjadi).
- Mkusanyiko wa msamiati unaambatana na ule ulio katika silabasi ya Kiswahili iliyoidhinishwa na taasisi ya elimu nchini (awali Kenya Institute of Education, sasa Kenya Institute of Curriculum Development).
- Kamusi hii ina picha maridadi zinazomvutia mwanafunzi na kumrahisishia kazi.
- Picha zote zimeambatanishwa na maelezo kabambe na kwa lugha nyepesi inayomfaa si mwanafunzi pekee bali mtu yeyote akipendaye Kiswahili.
- Msamiati uliotumika utamwezesha mwanafunzi kujua mengi kwenye mazingira yake.
-
My Storymoja book club diary
If you want to be smarter, more attractive and interesting, read more storybooks. If you want to be more creative so you can become an innovator or entrepreneur one day, read more storybooks. If you want a successful career and contribute to national development in the future, read more storybooks. Fill your diary every time you read. Show your parents or guardian your diary and tell them about what you read. Compare your diary with your friends and celebrate how many books you read. Reading empowers! Reading is cool! Reading is good for you!
READ WITH YOUR CHILD
Enjoy quality time with your child by reading together. Your child will love books for life and learn better if you follow these ten easy steps.
1. Read with your child in a quiet, relaxed setting such as bedtime.
2. Make it fun by reading the whole story with expression. Aim for the enjoyment of the story.
3. The next time you read the story, point to the words as you read.
4. Check for understanding by asking easy questions about the pictures, characters, and story, but please do not turn the session into an examination.
5. Find something to praise. Be positive. Shower your child with praise.
6. Read the same story on many occasions.
7. Over time, encourage your child to try and read the words or story to you.
8. Buy your child a variety of fun books such as picture books, comics, audiobooks and information books.
9. Show interest in what your child reads, ask questions and talk about stories you read in books.
10. Inspire your child to rate books highly. Let your child see you reading your own books. -
Kamusi ya Semi-Toleo Jipya by Ndalu,Kingei
by Ndalu, Kingei
Toleo Jipya Ia Kamusi ya Semi ndicho kitabu cha pekee kilichokusanya zaidi ya semi elfu nne. Kitabu hiki kinajumuisha semi, maana yake, pamoja na mifano faafu. Ufafanuzi wa msamiati umetiliwa maanani huku maana kadhaa za semi zikitolewa. Aidha, semi zilizomo humu kitabuni zimepangwa kialfabeti ili kurahisisha urejeleaji. Toleo hili Jipya Ia Kamusi ya Semi ni kitabu kinachowafaa wanafunzi na walimu wa kila daraja: shule za msingi, za upili na hata vyuo vikuu. Hii ni dafina kuu kwa wapenzi wote wa lugha na fasihi ya Kiswahili. Kitula King’ei ni mwalimu, mwandishi, mtafiti na msomi wa lugha na fasihi ya Kiswahili aliye na tajriba kubwa sana. Kwa sasa, ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Ahmed Ndalu amefundisha Kiswahili katika shule za upili na vyuoni, na vile vile kuandika vitabu kadhaa. Hivi sasa, amestaafu kazi ya ufundishaji na anajishughulisha na utafiti na uandishi wa vitabu vinavyoshughulikia nyanja tofauti tofauti za Kiswahili.
Shop By Categories
- International Curriculum
- Marketplace – Used Books!
- National Curriculum
- TVET/Higher Learning
- Lab Equipment
- General Books
- International Curriculum
- Marketplace – Used Books!
- National Curriculum
- TVET/Higher Learning
- Lab Equipment
- General Books