• OUP Kiswahili Dadisi Grade 1 Workbook

    by OUP Kenya


    Kiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha, Workbook ni mfululizo wa kipekee wa vitabu vya mazoezi katika mfumo mpya wa umilisi, Vitabu hivi vinaelekeza kikamilifu kufanya mazoezi ya lugha kwa njia ya kufurahisha na kuelimisha. Kila kitabu katika mfululizo huu kimefanyiwa utafiti wa kina na kuandikwa kwa ustadi ili kuwasaidia wanafunzi kupata umitisi wa msingi, ujuzi, maadili na kuwa na mitazamo bora maishani.

    ISBN: 9780195747362

  • OUP Kiswahili Dadisi Grade 3 Workbook

    Kiswahili Dadisi Mazoezi ya Lugha Workbook ni mfululizo wa kipekee wa vitabu vyo mazoezi katika mtalaa mpya wa umilisi. Kila kitabu katika mfululizo huu kimefanyiwa utafiti wa kina na kuandikwa kwa ustadi ili kuwasaidia wanafunzi kupata umilisi wa kimsingi, ujuzi, maadili na kuwa na mitazamo bora maishani. Vitabu hivi vinatoa utaratibu mwafaka wa kufanya mazoezi ya lugha kwa njia nyepesi na ya kueleweka.

  • OUP Kiswahili Dadisi Grade 5 Kitabu cha mwanafunzi (Approved)

    by Oxford

    Kiswahili Dadisi ni msururu wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa njia ya kipekee ili kutosheleza mahitaji ya mtalaa wa umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia stadi za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika, na vilevile sarufi. Aidha, vina mazoezi murua ambayo yatampa mwanafunzi hamu ya kujifunza. Pia vinakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala ibuka.
    Katika Kiswahili Dadisi, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 5, utapata:
    • mada zilizopangwa kwa kuzingatia muainisho wa mtalaa mpya.
    • mifano halisi ya miktadha ambapo lugha hutumika.
    • mazoezi ya kuwahamasisha wanafunzi kuendeleza ujifunzaji nje ya darasa na yale yenye kuwashirikisha katika shughuli za
    kijamii zinazokuza ujifunzaji.
    • mazoezi yanayomhusisha mwanafunzi moja kwa moja.
    • jinsi ya kuwashirikisha wazazi na walezi ili kuimarisha uwajibikaji.
    • vifungu vya kumburudisha na kumfikirisha mwanafunzi katika sehemu ya ‘Burudika’.
    Kiswahili Dadisi, Kitabu cha Mwanafunzi kina Mwongozo wa Mwalimu ambao pia una mazoezi na maelekezo tosha ambayo mwalimu atahitaji ili kumwongoza mwanafunzi aweze kufaulu katika mtalaa huu wa umilisi.

  • OUP Kiswahili Dadisi Grade 5 Mwalimu (Approved)

    by J. Ndege, E. Osoro and Z. Mucheria

    Kiswahili Dadisi Mwongozo wa Mwalimu, Gredi ya 5
    Kiswahili Dadisi ni msururu wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa njia ya kipekee ili kutosheleza mahitaji ya mtalaa wa umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunzi kupata umilisi wa lugha kupitia stadi za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika, na vilevile sarufi kama ilivyopendekezwa katika mtalaa.
    Vitabu katika msururu huu vina mazoezi murua ambayo yatamchangamsha mwanafunzi na kumpa hamu ya kujifunza lugha. Mazoezi haya yanakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala ibuka.
    Huu Mwongozo wa Mwalimu, Gredi ya 5, una mifano halisi na ya kutosha kumwezesha mwalimu kuwasaidia wanafunzi kukuza umilisi unaokusudiwa. Katika mwongozo huu, utapata:
    • utangulizi wa kina kuhusu mtalaa wa umilisi
    • muhtasari wa umilisi, maadili, masuala ibuka na shughuli nyinginezo zilizoratibiwa ufundishaji katika kila sura
    • matokeo maalumu, maandalizi ya somo na shughuli za ufunzaji wa kila somo mapendekezo ya majibu ya takribani maswali yote katika kitabu cha Mwanafunzi
    • mapendekezo ya shughuli za kutekelezwa na wanafunzi ili waendelee kujifunza wakiwa nje ya darasa
    • maswali ya ziada ili kukuwezesha kutathmini zaidi uelewa wa wanafunzi wako
    • maelekezo ya kina kuhusu jinsi ya kutathmini wanafunzi.

    Kiswahili Dadisi, Kitabu cha Mwanafunzi pamoja na Mwongozo wa Mwalimu vina shughuli, mazoezi na maelekezo tosha ambayo mwanafunzi na mwalimu wanahitaji ili kufaulu katika mtalaa huu wa umilisi.

  • OUP Kiswahili Dadisi Mazoezi Gradi 1 (Toleo Jipya)

    by OXFORD

    Kiswahili Dadisi ni msururu wa vitabu vilivyoandikwa kwa utaalamu na upekee ili kufanikisha ufundishaji na ujifunzaji wa mahitaji ya Mtaala wa Umilisi. Vitabu hivi vitawawezesha wanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia stadi za Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika, na vilevile Sarufi, kupitia mazoezi murua ambayo pia yanakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na
    kufahamisha kuhusu masuala mtambuko.

    Katika Kiswahili Dadisi, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya1 utapata:

    -mada zilizopangwa kwa kuzingatia muainisho wa mtaala.

    -mifano halisi ya matumizi ya lugha kimuktadha.

    -mazoezi ya kuchangamsha na kufikirisha ambayo yanawashirikisha wanafunzi moja kwa moja.

    -vifungu vya kuburudisha na vinavyoendeleza ujifunzaji.

    -nyimbo za kusisimua ambazo zitawachangamsha na kuwaburudisha wanafunzi.

    -picha za rangi, zenye mvuto wa kipekee na ambazo zinachangia pakubwa katika ujifunzaji wa mwanafunzi.

    -mazoezi ya kuwahamasisha wanafunzi kuendeleza ujifunzaji nje ya darasa.

    -mazoezi ambayo yatawashirikisha mwanafunzi kutumia vifaa vya kidijitali katika ujifunzaji.

    -jinsi ya kumshirikisha mzazi au mlezi kuimarisha ujifunzaji.

    ISBN: 9789914441383

  • OUP Kiswahili dadisi Mazoezi ya Lugha gredi 3 … by Waititu/Matei/Mbugua

    by Waititu/Matei/Mbugua
    Kiswahili Dadisi. Mazoezi ya Lugha ni msururu wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa upekee ili kutosheleza mahitaji ya mtalaa mpya wa Umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia stadi za kusikiliza. kuzungumza, kusoma na kuandika. Aidha. vina mazoezi murua ambayo yatampa mwanafunzi hamu ya kujifunza. Pia vinakuza umilisi iliopendekezwa. maadili no kufahamisha kuhusu masuala ibuka.
    Katika Kiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha. Kitabu cha Mwanafunzl. Gredi 3. utapata:
    • mada zilizopangwa kwa kuzingatia muainisho wa mtataa mpya
    • mifano halisi ya miktadha ambapo hutumika
    • mazoezi yanayomhusisha mwanafunzi moja kwa moja
    • jinsi ya kuwashirikisha wazazi na walezi iii kuimarisha uwajibikaji.

  • OUP Kiswahili Dadisi Workbook Grade 6

    by Oxford

    Kiswahili Dadisi Workbook ni msururu wa kipekee wa vitabu vya mazoezi katika Mtalaa wa Umilisi. Kila kitabu katika msururu huu kimefanyiwa utafiti wa kina na kuandikwa kwa ustadi ili kuwasaidia wanafunzi kupata umilisi wa kimsingi, ujuzi, maadili na kuwa na mitazamo bora maishani. Vitabu hivi vinatoa utaratibu mwafaka wa kufanya mazoezi ya lugha kwa njia nyepesi na ya kueleweka.

    Kitabu hiki:

    -kimeandikwa kwa kufuata utaratibu uliopendekezwa kwenye mtalaa

    – kina mazoezi mengi ya kuchangamsha na kuelimisha, na ambayo yatamwezeshamwanafunzi kujenga na kupanua umiliskatika kila mada.

    -kina dokezo ambazo zinatoa maelezo zaidi kuhusu vipengele lengwa.

    -kina tathmini ya binafsi ambayo itamsaidia mwanafunzi kukadiria umilisi wake katika mada ndogo zote.

    -kina majaribio ya mtihani wa mwisho wa elimu ya msingi.

  • OUP Kiswahili Fasaha Grade 8 (Approved)

    Kiswahili Fasaha ni msururu ulioandikwa kwa njia ya kipekee na unaokidhi mahitaji yote ya Mtaala wa Kiumilisi. Vitabu katika msururu huu vina shughuli anuwai ambazo zinalenga kumsaidia mwanafunzi kupata umilisi, maadili na masuala mtambuko
    yanayokusudiwa katika mtaala.

    Kiswahili Fasaha Kitabu cha Mwanafunzi Gredi ya 8 kina:

    -Shughuli mbalimbali zitakazomwezesha mwanafunzi kupata stadi zote nne za lugha – Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na
    Kuandika – pamoja na matumizi ya sarufi kimuktadha

    -Sehemu za Zinduo ambazo zinatoa maelezo ya kina kuhusu dhana husika

    -Sehemu za Elimujamii ambazo zinampa mwanafunzi nafasi ya kuendeleza ujifunzaji wake nje ya darasa

    -Sehemu za Dijitika ambazo kwazo mwanafunzi ana nafasi ya kutangamana na vifaa vya kidijitali katika kufanya mazoezi

    -Michoro ya rangi inayochangia uelewa wa dhana zinazofunzwa

    -Tathmini binafsi baada ya kila mada kuu ili kumsaidia mwanafunzi kupima uelewa wake wa dhana husika

    -Sehemu ya Tafakari mwishoni mwa kila suala kuu, ambayo inalenga kumpa mwanafunzi ari ya kutumia aliyojifunza ili kuboresha hali yake na ya jamii nzima.

  • OUP Kiswahili Fasaha Kitabu cha Mwalimu Grade 8 (Approved)

    Kiswahili Fasaha ni msururu ulioandikwa kwa njia ya kipekee na unaokidhi mahitaji yote ya Mtaala wa Kiumilisi. Vitabu katika msururu huu vina shughuli anuwai ambazo zinalenga kumsaidia mwanafunzi kupata umilisi, maadili na masuala mtambuko yanayokusudiwa katika mtaala.

    Mwongozo huu wa mwalimu una:

    -Utangulizi kuhusu Mtaala wa Kiumilisi

    -Muhtasari wa umilisi, maadili na masuala mtambuko yaliyoratibiwa kukuzwa

    -Mifano ya vifaa vya kutathmini na jinsi ya kuviandaa vifaa hivyo

    -Mapendekezo kuhusu mbinu bora za ufunzaji na ujifunzaji

    -Jinsi ya kuwahudumia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

    -Nyaraka za kitaaluma

    -Maelekezo kuhusu jinsi ya kuwahusisha wanafunzi katika shughuli za kijamii.

    Mwongozo huu pamoja na Kiswahili Fasaha Kitabu cha Mwanfunzi Gredi ya 8 ni nyenzo muhimu zitakazokuwezesha wewe na wanafunzi wako kufaulu katika Mtaala wa Kiumilisi.

Main Menu