• Kurunzi ya Insha Kidato cha 1 na 2 by Spotlight Publishers

    by Spotlight Publishers

    Kurunzi ya Insha: Kidato cha I na 2, kimezingatia tungo zote za ubunifu/kawaida na za kiuamilifu zilizomo kwenye silabasi ya Kiswahili, kidato cha kwanza na pili. Kinawapa wanafunzi mwangaza na ustadi kamili kuhusu uandishi wa tungo hizi kwa kutilia mkazo masharti ya karatasi ya insha katika mtihani wa KCSE. Chapisho hili ni kito kwa mwanafunzi anayetafuta alama ‘A’ katika mtihani. Mwalimu amepewa dira ya kufundishia na kutathminia uwezo wa wanafunzi wake katika uandishi wa insha.
    Yaliyomo kitabuni:
    • Kitabu hiki kina sura tatu kuu zinazoangazia tungo zote zinazofaa kushughulikiwa katika kidato cha kwanza na pili.
    • Sura ya kwanza inaangazia mambo ya jumla ambayo ni lazima mwanafunzi ayazingatie anapoandika insha yoyote. Mambo haya pia ndiyo huzingatiwa na mwalimu anapofundisha darasani. Vilevile, mambo haya ndiyo dira ya kusahihisha insha katika mtihani wa KCSE. Dhamira ya sura hii ni kumsaidia mwanafunzi kutambua makosa ambayo aghalabu humbomoa na kumpunguzia alama.
    • Sura ya pili inashughulikia insha za kubuni/kawaida. Hizi ni insha zinazotathmini
    ubunifu wa mwanafunzi.
    • Sura ya tatu inaangazia insha za kiuamilifu. Tungo hizi huandikwa kwa kufuata sheria, maumbo au taratibu zilizowekwa. • Muundo na sifa za kila insha zimeelezwa kwa kina.
    • Makosa ya kawaida yanayofanywa na watahiniwa wanapoandika insha yametajwa ili kuwatahadharisha waepukane nayo.
    • Upekee wa kitabu hiki ni kuwepo kwa mifano miwili miwili ya insha zilizoandikwa na waandishi wa kitabu hiki. Pia, mifano mitatu mitatu ya insha zilizoandikwa na wanafunzi wa kidato cha l na 2, katika mazingira ya mtihani, kutoka shule mbalimbali nchini imeambatishwa. Insha hizi zimesahihishwa na watahini wa kiwango cha kitaifa kulingana na utaratibu unaozingatiwa katika kusahihisha mitihani ya KCSE. Maoni kuhusu jinsi ya kuziimarisha yametolewa.
    • Zoezi limetolewa baada ya kila utungo ili mwalimu na mwanafunzi waweze kulitumia kufanyia mazoezi darasani. Vielelezo vya mtihani wa insha wa KCSE vimetolewa ili mwanafunzi apate taswira kamili ya jinsi mtihani wa insha unavyoandaliwa na pia ajiandae kuukabili

  • Kurunzi ya Insha Kidato cha 1 na 2 by Spotlight Publishers

    by Spotlight Publishers

    Kurunzi ya Insha: Kidato cha I na 2, kimezingatia tungo zote za ubunifu/kawaida na za kiuamilifu zilizomo kwenye silabasi ya Kiswahili, kidato cha kwanza na pili. Kinawapa wanafunzi mwangaza na ustadi kamili kuhusu uandishi wa tungo hizi kwa kutilia mkazo masharti ya karatasi ya insha katika mtihani wa KCSE. Chapisho hili ni kito kwa mwanafunzi anayetafuta alama ‘A’ katika mtihani. Mwalimu amepewa dira ya kufundishia na kutathminia uwezo wa wanafunzi wake katika uandishi wa insha.
    Yaliyomo kitabuni:
    • Kitabu hiki kina sura tatu kuu zinazoangazia tungo zote zinazofaa kushughulikiwa katika kidato cha kwanza na pili.
    • Sura ya kwanza inaangazia mambo ya jumla ambayo ni lazima mwanafunzi ayazingatie anapoandika insha yoyote. Mambo haya pia ndiyo huzingatiwa na mwalimu anapofundisha darasani. Vilevile, mambo haya ndiyo dira ya kusahihisha insha katika mtihani wa KCSE. Dhamira ya sura hii ni kumsaidia mwanafunzi kutambua makosa ambayo aghalabu humbomoa na kumpunguzia alama.
    • Sura ya pili inashughulikia insha za kubuni/kawaida. Hizi ni insha zinazotathmini
    ubunifu wa mwanafunzi.
    • Sura ya tatu inaangazia insha za kiuamilifu. Tungo hizi huandikwa kwa kufuata sheria, maumbo au taratibu zilizowekwa. • Muundo na sifa za kila insha zimeelezwa kwa kina.
    • Makosa ya kawaida yanayofanywa na watahiniwa wanapoandika insha yametajwa ili kuwatahadharisha waepukane nayo.
    • Upekee wa kitabu hiki ni kuwepo kwa mifano miwili miwili ya insha zilizoandikwa na waandishi wa kitabu hiki. Pia, mifano mitatu mitatu ya insha zilizoandikwa na wanafunzi wa kidato cha l na 2, katika mazingira ya mtihani, kutoka shule mbalimbali nchini imeambatishwa. Insha hizi zimesahihishwa na watahini wa kiwango cha kitaifa kulingana na utaratibu unaozingatiwa katika kusahihisha mitihani ya KCSE. Maoni kuhusu jinsi ya kuziimarisha yametolewa.
    • Zoezi limetolewa baada ya kila utungo ili mwalimu na mwanafunzi waweze kulitumia kufanyia mazoezi darasani. Vielelezo vya mtihani wa insha wa KCSE vimetolewa ili mwanafunzi apate taswira kamili ya jinsi mtihani wa insha unavyoandaliwa na pia ajiandae kuukabili.

  • Kurunzi ya Kiswahili Grade 5 Mwanafunzi (Approved)

    by A.Matei, F.Atulo, F.Wangome

    Kurunzi ya Kiswahili Kitabu cha Mwanafunzi Gredi ya 5 kimeandaliwa kwa ustadi ili kumwezesha mwanafunzi kumudu mtalaa huu unaolenga umilisi kwa njia sahili, yenye mvuto na ya kumjumuisha moja kwa moja kwenye shughuli za ufunzaji.
    Kitabu hiki
    • Kimeshughulikia mada kwa njia inayomwezesha mwanafunzi kushiriki kikamilifu katika ujifunzaji.
    • Mada na shughuli za darasani zimeteuliwa kwa uangalifu kumjengea mwanafunzi umilisi wa aina mbalimbali. Mada hizi zinalenga kuimarisha umilisi wa kusikiliza kwa makini, kuzungumza kwa ujasiri, kusoma kwa ufasaha na kuandika vyema.
    • Kuna mazoezi na mijarabu kama vile shughuli kwa mwanafunzi, shughuli ya vikundi, kazimradi, shughuli ya nyumbani na michezo ili kumwezesha mwalimu kupima umilisi wa mwanafunzi kwenye stadi mbalimbali za lugha.
    • Picha halisi na michoro ya kuvutia inamsaidia mwanafunzi katika uelewa wa mada.
    • Kinalenga kumsaidia mwanafunzi kutumia vifaa vya teknolojia kama vile video, redio, tabuleti katika kurahisisha ujifunzaji.
    • Mbinu tofauti za ufunzaji zimejumuishwa kama vile miradi ya uwekezaji, shughuli nje ya darasa, kutumia nyimbo, mashairi, kumhusisha mzazi au mlezi na ujifunzaji katika vikundi. Mbinu hizi zinasaidia kujenga umilisi wa mwanafunzi.
    • Masuala mtambuko na kuhusisha maadili kujenga mada tofauti imeshughulikiwa.

  • Kurunzi ya Kiswahili Grade 7

    by Spotlight

    Kurunzi ya Kiswahili Kitabu cha Mwanafunzi Gredi ya 7 kimeandaliwa kwa ustadi ili kumwezesha mwanafunzi kumudu mtaala mpya unaolenga umilisi kwa njia sahili, yenye mvuto na ya kumjumuisha moja kwa moja kwenye shughuli za ufunzaji.

  • Kurunzi ya Kiswahili Kitabu cha Mwanafunzi

    Kurunzi ya Kiswahili Kitabu cha Mwanafunzi Gredi ya Nne kimeandaliwa kwa ustadi ili kumwezesha mwanafunzi kumudu mtaala huu unaolenga umilisi kwa nijia sahili, yenye mvuto na ya kumjumuisha moja kwa moja kwenye shughuli za ujifunzaji.

    Kitabu hiki:

    * Kimeshughulikia mada kwa namna ambayo inamwezesha mwanafunzi kushiriki kikamilifu katika ujifunzaji.

    * Mada na shughuli za ujifunzaji zimeteuliwa kwa uangalifu ili kumjengea mwanafunzi umilisi wa aina mbalimbali.

    * Kina mazoezi na mijarabu anuwai ya kumtathmini mwanafunzi.

    * Kina picha halisi na michoro ya kuvutia inayosaidia katika uelewa wa mada.

    * Kinalenga kumsaidia mwanafunzi kutumia vifaa vya teknolojia kama vile video, redio na tabuleti katika kurahisisha ujifunzaji.

    *  Mbinu tofauti za ujifunzaji zimejumuishwa kama vile kazi mradi, shughuli nje ya darasa, kumwalika mgeni, kutumia nyimbo, mashairi, kumhusisha mzazi au mlezi, uchoraji na ujifunzaji katika vikundi. Mbinu hizi zinasaidia kuujenga umilisi wa mwanafunzi.

    * Mada na shughuli za ujifunzaji zimeshughulikia masuala mtambuko na kumsisitizia mwanafunzi maadili.

    * Kitebu cha mwalimu kipo ili kumpa mapendekezo katika ufunzaji.

  • Kurunzi ya Marejeleo Halahala Kiswahili 8 Toleo jipya …

    Kurunzi ya Marejeleo Halahala Kiswahili 8 kimeandaliwa maalum ili kiwasaidie zaidi wanafunzi wa darasa la 8 katika mazoezi na marudio ya silabasi ya darasa la 8 na pia kujitayarisha vyema kwa mtihani wa KCPE. Ni kifaa muhimu kwa walimu wanaohitaji maswali tofauti tofauti yanayoweza kutumika kwa mazoezi ya darasani, mitihani ya mwisho wa muhula na mitihani ya majaribio ya KCPE.

Main Menu