OUP Kiswahili Fasaha Grade 8 (Approved)
KShs880.00
Kiswahili Fasaha ni msururu ulioandikwa kwa njia ya kipekee na unaokidhi mahitaji yote ya Mtaala wa Kiumilisi. Vitabu katika msururu huu vina shughuli anuwai ambazo zinalenga kumsaidia mwanafunzi kupata umilisi, maadili na masuala mtambuko
yanayokusudiwa katika mtaala.
Kiswahili Fasaha Kitabu cha Mwanafunzi Gredi ya 8 kina:
-Shughuli mbalimbali zitakazomwezesha mwanafunzi kupata stadi zote nne za lugha – Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na
Kuandika – pamoja na matumizi ya sarufi kimuktadha
-Sehemu za Zinduo ambazo zinatoa maelezo ya kina kuhusu dhana husika
-Sehemu za Elimujamii ambazo zinampa mwanafunzi nafasi ya kuendeleza ujifunzaji wake nje ya darasa
-Sehemu za Dijitika ambazo kwazo mwanafunzi ana nafasi ya kutangamana na vifaa vya kidijitali katika kufanya mazoezi
-Michoro ya rangi inayochangia uelewa wa dhana zinazofunzwa
-Tathmini binafsi baada ya kila mada kuu ili kumsaidia mwanafunzi kupima uelewa wake wa dhana husika
-Sehemu ya Tafakari mwishoni mwa kila suala kuu, ambayo inalenga kumpa mwanafunzi ari ya kutumia aliyojifunza ili kuboresha hali yake na ya jamii nzima.
Reviews
There are no reviews yet.