KLB Visionary Mazoezi ya Kiswahili GD3 Trs (Appr) by Atibu Bakari

KShs465.00

In stock

by Atibu Bakari
KLB Mazoezi ya Kiswahiil Gredi ya Tatu (Mwongozo wa Mwalimu) ni kitabu mojawapo kati ya vitabu vinavyochapishwa na Kenya Literature Bureau vya msururu wa KLB Visionary. Msururu huu wa vitabu umezingatia Mtalaa wa kiumilisi wa mwaka wa 2017 wa masomo ya shule za msingi. Kitabu hiki kimekusudiwa kumwezesha mwanafunzi kukuza uwezo wa kutumia stadi zote nne za lugha ya Kiswahili; Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika. Kupitia stadi hizi, mwanafunzi anakuza uwezo wake wa lugha.
Toleo hili limejumuisha mambo muhimu ambayo yanachangia ujifunzaji wa sasa ambayo ni masuala mtambuko, maswali dadisi, masuala ya  jinsia, utendaji wa mwanafunzi, picha murua za kuchangamsha na kuibua hamu ya kudadisi kwa mwanafunzi na mbinu tofauti za kumwezesha mwanafunzi kukuza uwezo wake wa kujifunza. Mazingira halisi ya mwanafunzi yamezingatiwa katika kukuza kazi hii. Hili linamwezesha mwanafunzi kujifunza katika hali halisi. Lugha sahili imetumika ili kurahisisha kuelewa kwa mada zote katika kitabu.
Msururu huu wa KLB Visionary umeshughulikiwa na jopo la walimu stadi wenye tajriba_ maalum katika kiwango cha shule ya msingi cha ujifunzaji. Kitabu hiki kimetolewa pamoja na Kitabu cha Mwanafunzi ambacho kitamwezesha mwalimu au msaidizi wa mwanafunzi kushughulikia kikamilifu mada zote zilizoko kwenye mtalaa.

Compare
Category:
Be the first to review “KLB Visionary Mazoezi ya Kiswahili GD3 Trs (Appr) by Atibu Bakari”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Reviews

There are no reviews yet.

See It Styled On Instagram

    No access token
Show Buttons
Hide Buttons

Main Menu

1
Scan the code
Thank you for visiting us,

Need any help?