-
Kamusi Elezi ya Kiswahili (JKF) by JKF
Kamusi Elezi ye Kiswahili ni kamusi ya kisasa iliyoandikwa kwa ufindi wa kipekee na iliyo na maelezo ya vidahizo, Na kamusi iliyofungamana na hatua za kimaendeleo katika taaluma ya lugha ya Kiswahili na fasihi yake Itawafaa wataalamu, wanafunzi na walumizi wengine wa lugha ya Kiswahili. NI kamusi yenye upeo wa kimataifa. Licha ya maneno, semi na maelezo yake, ina vielezo vya michoro na matamshi ya vidahizo
Site kuu za Kamusi Elezi ya Kiswahlli • Vidahizo vipatavyo 45,000 • Maneno mapya yapatayo I.000 • Jopo la wataalamu wenye tajiriba kutoka Kenya. Tanzania na Japani • Matamshi murua kifonetiki: kulingana na alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa • maelezo kamilifu ya kidahizo bila kutengemea visawe• Ufafanuzi wa kipekee wa methali, misemo na nahau • Kuhusishwa kwa dhana mpya za teknolopa na sayansi • msamiati mpya wa samaki na vyombo vya bahari • Mifano mwalaka yenye kushadidia maana • michoro na picha maridhawa zinazooana na maelezo
-
Kamusi Fafanuzi ya Methali by Timothy Arege,Mwalaa Nya…
by Timothy Arege, Mwalaa Nyanje
Kamusi Fafanuzi ya Methali ni kitabu muhimu sana kwa wanafunzi na walimu wa shule za msingi na upili. Kitawafaa wanafunzi wa vyuo vya ualimu na vyuo vikuu pamoja na watafiti na wapenzi wa lugha ya Kiswahili katika viwango vyote. -
Kamusi Rasmi ya Picha by Yahya Mutuku
by Yahya Mutuku
Kamusi rasmi ya picha imeandikwa kwa upekee usiodhihirika katika kamusi nyingine. Kamusi hii ina sifa zifuatazo- Imeepuka mpangilio wa kialfabeti uliotumiwa na kamusi nyingine. Msamiati umepangwa kwa makundi badala ya kialfabeti kwa sababu wanafunzi katika kiwango hiki bado hawawezi kusaka msamiati kialfabeti (kiabjadi).
- Mkusanyiko wa msamiati unaambatana na ule ulio katika silabasi ya Kiswahili iliyoidhinishwa na taasisi ya elimu nchini (awali Kenya Institute of Education, sasa Kenya Institute of Curriculum Development).
- Kamusi hii ina picha maridadi zinazomvutia mwanafunzi na kumrahisishia kazi.
- Picha zote zimeambatanishwa na maelezo kabambe na kwa lugha nyepesi inayomfaa si mwanafunzi pekee bali mtu yeyote akipendaye Kiswahili.
- Msamiati uliotumika utamwezesha mwanafunzi kujua mengi kwenye mazingira yake.
-
Kamusi ya Karne ya 21
by EMAC BAKITA
Kamusi inayoakisi Maendeleo na Masuala Ibuka ya lugha ya Kiswahili
Vidahizo vipatavyo 42,000. -
-
Kamusi ya picha by K w wamitila
Kamusi ya Picha ni kitabu muhimu kwa wanafunzi wanaojifunza lugha ya Kiswahili kwa sababu ya upekee wake. Kamusi hii imejumuisha picha safi na vielelezo vingi na vya kupendeza. Picha halisi zimetumiwa katika baadhi ya sehemu ili msomaji aweze kusawiri vizuri picha ya kitu halisi. Aidha imepangiliwa kwa namna ambayo itawafaa wanafunzi wachanga. Kamusi hii, bila shaka, ni nyenzo muhimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na za sekondari pia.
-
Kamusi ya Semi-Toleo Jipya by Ndalu,Kingei
by Ndalu, Kingei
Toleo Jipya Ia Kamusi ya Semi ndicho kitabu cha pekee kilichokusanya zaidi ya semi elfu nne. Kitabu hiki kinajumuisha semi, maana yake, pamoja na mifano faafu. Ufafanuzi wa msamiati umetiliwa maanani huku maana kadhaa za semi zikitolewa. Aidha, semi zilizomo humu kitabuni zimepangwa kialfabeti ili kurahisisha urejeleaji. Toleo hili Jipya Ia Kamusi ya Semi ni kitabu kinachowafaa wanafunzi na walimu wa kila daraja: shule za msingi, za upili na hata vyuo vikuu. Hii ni dafina kuu kwa wapenzi wote wa lugha na fasihi ya Kiswahili. Kitula King’ei ni mwalimu, mwandishi, mtafiti na msomi wa lugha na fasihi ya Kiswahili aliye na tajriba kubwa sana. Kwa sasa, ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Ahmed Ndalu amefundisha Kiswahili katika shule za upili na vyuoni, na vile vile kuandika vitabu kadhaa. Hivi sasa, amestaafu kazi ya ufundishaji na anajishughulisha na utafiti na uandishi wa vitabu vinavyoshughulikia nyanja tofauti tofauti za Kiswahili. -
Kamusi ya Visawe by EAEP
Kamusi ya Visawe
Swahili Dictionary of Synonyms
Kamusi ya Visawe ni kamusi ya kwanza kushughulikiwa na kuchapishwa katika Kiswahili kwa madhumuni ya kutoa tafsiri ya neno fulani kwa kupata neno ama maneno mengine yenye maana halisi au yenye maana halisi au yenye maana ya karibu na neno linalotafsiriwa.
Kamusi hii imekusanya vidahizo visivyopungua 14,000 vingine vikiwa na visawe vine na zaidi. Kamusi hii pia imejaribu kuonyesha hall tofauti tofauti za vidahizo kama vile vitenzi au jina. Kwa hivyo, ni wazi kuwa lugha ya Kiswahili imejaa utajiri mwingi wa msamiati na mtumiaji yeyote wa lugha hii, anayetumia Kamusi ya visawe, hana haja ya kutapatapa kujieleza kwani atakuwa amesheheni maneno tele yenye maana moja.
Kamusi hii ni akiba kubwa yenye manufaa mengi hasa kwa wanafunzi wa shule za msingi, shule za upili, Vyuo Vikuu na pia kwa walimu na wanafunzi wa lugha ya Kiswahili popote pengine.
Mohammed Abdulla Mohamed alizaliwa Zanzibar na kusomea huko huko. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salamu na kupata shahada ya BA Hons na MA katika Elimu. Baadaye alijiunga na Chuo kikuu cha Columbia ambapo alipata shahada ya Ph.d katika isimu ya kufundisha. Alipata shahada ya MSc (Hons) katika Chuo Kikuu cha New York baadaye. Pia amewahi kuwa mhadhiri katika vyuo mbalimbali nchini Tanzania na Kenya.
Said A. Mohamed alizaliwa Ugunja mwaka wa 1947. Alisomea huko huko na kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Kisha Chuo Kikuu cha Leipzig, Ujerumani. Amefundisha katika shule za upili na Vyuo mbalimbali.
Usanifu wa jalada: Adrian Kheri Yongo
East African Educational Publishers Ltd
Nairobi. Kampala .Dar es Salaam • Kigali
Kamusl ya Vlsawe
Shop By Categories
- International Curriculum
- Marketplace – Used Books!
- National Curriculum
- TVET/Higher Learning
- Lab Equipment
- General Books
- International Curriculum
- Marketplace – Used Books!
- National Curriculum
- TVET/Higher Learning
- Lab Equipment
- General Books