Kielekezi cha Marudio ya Kiswahili 3
KShs500.00
by A.litinyu, C.Kiini, M.Kemunto, N.Musyimi.
KIELEKEZI cha Marudio ya Kiswahili 3 kimeandikwa Hi kuwasaidia wanafunzi wa shule za msingi nchini Kenya kufanya marudio ya silabasi ya Kiswahili ya darasa la tatu.KIELEKEZI cha Marudio ya Kiswahili 3:Kimezingatia kikamilifu silabasi ya Kiswahili ya darasa la tatu kama ilivyoandikwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitalaa ya Kenya.Kimewasilisha yaliyomo katika lugha nyepesi ambayo mwanafunzi anaweza kuelewa kwa urahisi. Kimetumia michoro mbalimbali ya kuvutia na inayofafanua yaliyomo.Kina zoezi moja au zaidi mwishoni mwa kila mada ili kumsaidia mwanafunzi kufanya marudio ya mada hiyo.Kina zoezi moja la jumla mwishoni mwa kila sura ili kumsaidia mwanafunzi kufanya marudio ya sura yote.Kina karatasi nne za marudio kumsaidia mwanafunzi kufanya marudio ya silabasi yote ya darasa la tatu na kujiandaa vilivyo kwa mtihani wake.Kimepangwa kwa utaratibu na ubunifu mkubwa ili kunasa akili za mwanafunzi.Kina majibu katika kijitabu tofauti ambacho kinajumuisha majibu ya maswali yote ya Somo la Kiingereza, Somo la Kiswahili, Somo la Hisabati, Somo la Sayansi, Somo la Jamii na Somo la Dini. Lengo la hatua hii ni kumsaidia mwanafunzi kufanya kazi yake bila ya au kabla ya kutazama majibu na wala sio kunakili majibu tu.
Reviews
There are no reviews yet.