-
Get it Right Kiswahili Kidato 1 na 2 marudio
by Kamithi
GET IT RIGHT KISWAHILI KIDATO CHA 1 NA 2 ni kitabu kilichoandikwa kwa ustadi wa kupigiwa mfano. Maarubu ya kitabu hiki ni kuwajengea wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili, msingi thabiti wa kukabiliana na mtihani wa kitaifa (K.C.S.£). Aidha, ni kitabu ambacho kitawafaa pakubwa wanafunzi wa kidato cha tatu na cha nne, wanaotaka kujikumbusha stadi zilizofunzwa katika kidato cha kwanza na cha pili. Kimeandikwa kwa mtindo mwepesi na rahisi kusomeka.
Kitabu hiki kina sifa zifuatazo:
- Â Kimeshughulikia stadi zote zinazostahili kufunzwa katika kidato cha kwanza na cha pili kwa mujibu wa silabasi.
- Kina maelezo ya utondoti ambayo yametolewa kwa lugha rahisi inayowawezesha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili kuelewa fika vipengele vyote vya: ufahamu, muhtasari, matumizi ya lugha, uandishi wa insha na tungo za kiuamilifu, fasihi simulizi, fasihi andishi na ushairi bila usaidizi wa mwalimu.
- Kimetoa mifano maridhawa kwa kila stadi pamoja na mazoezi tele baada ya kila mada ndogo na mada kuu. Aidha, majibu ya mazoezi haya yametolewa ili kurahisisha marudio na uelewa wa mwanafunzi.
- Kina mitihani kielelezo inayolenga kunoa makali ya mwanafunzi. Majibu ya mitihani hii yamo kitabuni kwenye kurasa za mwisho.
- Mwandishi wa kitabu hiki ni mwalimu mwenye tajriba pevu ya kufundisha Kiswahili. Amefundisha katika shule mbalimbali humu nchini na kupata matokeo bora katika mitihani ya kitaifa.
ISBN: 9789966193421
-
Marudio Hima Hima Kiswahili kidato cha 2 (maswali,Majibu,Mazoezi … by Dinah S.Osango
by Dinah S.Osango
Marudio Hima Hima Kiswahili Kidato cha 2 ni kitabu cha pili cha marudio katika msururu wa vitabu vinne vya kidato cha kwanza hadi cha nne vya marudio.Vitabu hivi vimetungwa kwa kuzingatia mahitaji ya silabasi pamoja na kumwelekeza mwanafunzi na mwalimu katika kuyaelewa mahitaji kamili ya kila swali. Kinyume na kawaida katika vitabu vya mazoezi na marudio, msururu wa Marudio Hima Hima unazingatia:
Huu ni msururu wa vitabu ambavyo ni kama vito vya thamana katika kumtayarisha mwanafunzi kukumbana na mtihani wa Kiswahili katika ngazi ya KCSE.Waandishi wa msururu huu ni walimu waliobobea na wenye tajriba. Wamefundisha Kiswahili kwa miaka mingi pamoja na kushiriki katika utungaji na utahini wa mtihani wa Kiswahili wa KCSE. -
Alive: A New CRE course Form 2 by Petronilla Kidakwa, Jane…
by Petronilla Kidakwa, Jane Mbugua, Evelyn Jaoko, Daniel Mirumbe
ALIVE: A New Christian Religious Education Course is a series that comprehensively addresses the objectives and requirements of the Christian Religious Education CRE Syllabus for secondary schools. Developed by a team of subject experts and experienced teachers, this innovative series combines knowledge acquisition with fun elements and real-life occurrences to deliver on exciting top-notch learning experience. This series aims at moulding learners into role models in society by instilling positive behavioural change. It also helps them to develop a good attitude and life skills that will enable them to effectively deal with emerging issues. The Student’s Book for Form 2 is skilfully written to enhance the learners’ understanding of the main concepts of the CRE course. It also guides the learners on how to incorporate the concepts and lessons learned in their daily lives. -
Kurunzi ya Insha Kidato cha 1 na 2 by Spotlight Publishers
by Spotlight Publishers
Kurunzi ya Insha: Kidato cha I na 2, kimezingatia tungo zote za ubunifu/kawaida na za kiuamilifu zilizomo kwenye silabasi ya Kiswahili, kidato cha kwanza na pili. Kinawapa wanafunzi mwangaza na ustadi kamili kuhusu uandishi wa tungo hizi kwa kutilia mkazo masharti ya karatasi ya insha katika mtihani wa KCSE. Chapisho hili ni kito kwa mwanafunzi anayetafuta alama ‘A’ katika mtihani. Mwalimu amepewa dira ya kufundishia na kutathminia uwezo wa wanafunzi wake katika uandishi wa insha.
Yaliyomo kitabuni:
• Kitabu hiki kina sura tatu kuu zinazoangazia tungo zote zinazofaa kushughulikiwa katika kidato cha kwanza na pili.
• Sura ya kwanza inaangazia mambo ya jumla ambayo ni lazima mwanafunzi ayazingatie anapoandika insha yoyote. Mambo haya pia ndiyo huzingatiwa na mwalimu anapofundisha darasani. Vilevile, mambo haya ndiyo dira ya kusahihisha insha katika mtihani wa KCSE. Dhamira ya sura hii ni kumsaidia mwanafunzi kutambua makosa ambayo aghalabu humbomoa na kumpunguzia alama.
• Sura ya pili inashughulikia insha za kubuni/kawaida. Hizi ni insha zinazotathmini
ubunifu wa mwanafunzi.
• Sura ya tatu inaangazia insha za kiuamilifu. Tungo hizi huandikwa kwa kufuata sheria, maumbo au taratibu zilizowekwa. • Muundo na sifa za kila insha zimeelezwa kwa kina.
• Makosa ya kawaida yanayofanywa na watahiniwa wanapoandika insha yametajwa ili kuwatahadharisha waepukane nayo.
• Upekee wa kitabu hiki ni kuwepo kwa mifano miwili miwili ya insha zilizoandikwa na waandishi wa kitabu hiki. Pia, mifano mitatu mitatu ya insha zilizoandikwa na wanafunzi wa kidato cha l na 2, katika mazingira ya mtihani, kutoka shule mbalimbali nchini imeambatishwa. Insha hizi zimesahihishwa na watahini wa kiwango cha kitaifa kulingana na utaratibu unaozingatiwa katika kusahihisha mitihani ya KCSE. Maoni kuhusu jinsi ya kuziimarisha yametolewa.
• Zoezi limetolewa baada ya kila utungo ili mwalimu na mwanafunzi waweze kulitumia kufanyia mazoezi darasani. Vielelezo vya mtihani wa insha wa KCSE vimetolewa ili mwanafunzi apate taswira kamili ya jinsi mtihani wa insha unavyoandaliwa na pia ajiandae kuukabili -
KCSE Made Familiar: Mathematics Workbook 1995-2021 (New Edition)
by Caroline Njenga
KC.S.E Made Familiar workbooks are a series of revision books meant to make K.C.S.E. familiar to leaners.
The benefits of these workbook to learners are immense and always result in improved grades. Some of the benefits include:
* provision of past K.C.S.E. questions in their original form, arranged in topics,
and in the respective forms in which the topics are taught.
* provision of answers, which help learners to work independently.
* exposure of learners to exam-type questions in various topics, thus helping
learners to :
✓ internalize concepts by practicing questions from topics already taught in class.
✓ relate what they are taught in class with K.C.S.E. thereby making K.C.S.E. questions familiar.
✓ identify their weak areas and aim to continually improve in these areas.
✓ build confidence through answering/working out questions in any given topic.
* Helping teachers make revision easy and interesting to learners.ISBN: 9789966055071
-
High Flyer Series Combined Art Subjects Form 2 by David mwangi
by David mwangi
Contains questions, answers and exercises to guide in exam preparation for success in Secondary school education examinations
Shop By Categories
- International Curriculum
- Marketplace – Used Books!
- National Curriculum
- TVET/Higher Learning
- Lab Equipment
- General Books
- International Curriculum
- Marketplace – Used Books!
- National Curriculum
- TVET/Higher Learning
- Lab Equipment
- General Books