Tadubiri za Insha Darasa la 5:Mbinu na Mapambo

KShs510.00

In stock

by Tsalwa Abubakar, John M.ngeera

Tadubiri za Insha: Mbinu na Mapambo, Darasa la 5 ni kitabu kilichoandikwa kwa ustadi na ubunifu wa hali ya juu kwa madhumuni ya kukidhi mahitaji ya wanafunzi na walimu katika shule za msingi – darasa la tano. Lugha iliyotumika ni rahisi kueleweka na wanafunzi wote kutoka mazingira mbalimbali.Waandishi wa kitabu hiki ni walimu stadi wenye tajriba pana ya kufundisha na kutahini Kiswahili – ngazi ya KCPE kwa miaka mingi. Wameangazia kwa undani na kwa mapana na marefu mikakati, mbinu, taratibu, dhana, kunga, miundo, mapambo na vipengele vinginevyo muhimu katika uandishi wa insha za kuvutia na za kuzoa alama za juu zaidi. Hii ni kwa kuhakikisha kwamba kitabu hiki kitamwezesha mwanafunzi kuandika insha kwa namna na mtindo faridi wenye mnato wa kipekee.Mifano kadha ya insha mbalimbali imetolewa katika kitabu hiki ili kurahisisha uelewaji wa maelezo yaliyomo na pia kushadidia hoja muhimu.

Compare
Be the first to review “Tadubiri za Insha Darasa la 5:Mbinu na Mapambo”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Reviews

There are no reviews yet.

See It Styled On Instagram

    No access token
Show Buttons
Hide Buttons

Main Menu

1
Scan the code
Thank you for visiting us,

Need any help?