Moran Stadi za Kiswahili Mwalimu GD3 (Approved) by Kipande

KShs360.00

In stock

by Kipande
Stadi za Kiswahili, Kitabu cha Mwalimu, Gredi ya 3 ni mwongozo unaomwelekeza mwalimu kuendesha vipindi vya Kiswahili darasani. Kwa mintarafu ya mtaala mpya uegemedo umilisi uliozinduliwa na Taasisi ya Ukuzgji Mitaala ya Kenya (KICD) mnamo Septemba 2017 na uliotumiwa kukiandaa kitabu hiki, mwalimu ni mwezeshaji wa mchakato wa ufundishgji na ujifunzaji. Mwongozo huu umetayarishwa kwa kutilia maanani ukweli huu.
Mwalimu amependekezewa jinsi ya kuandaa masomo, mbinu, zana na vifaa, utaratibu wa ufundishaji na jinsi ya kupima kiwango cha umilisi wa mwanafunzi baada ya kila kipindi. Aidha, Mwalimu amependekezewa jinsi ya kusimamia shughuli za mwanafunzi binafsi, za wanafunzi wawiliwawili na hata za makundi ya wanafunzi. Aidha, majibu ya mazoezi yaliyomo katika Kitabu cha Mwanafunzi yametolewa katika mwongozo huu.

Katika kila kipindi, mwalimu amependekezewa jinsi ya kuhusisha stadi nne kuu za lugha: kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika. Si hayo tu, ameelekezwa jinsi ya kuoanisha mada mbalimbali na umilisi wa kimsingi, masuala mtambuko, maadili, uhusiano wa mada mbalimbali na masomo mengine miongoni mwa masuala mengine yanayofumbatwa na mtaala mpya uegemedo umilisi.

Azma ya mwongozo huu ni kumchochea mwalimu kuwa mbunifu katika kuendeleza vipindi vya Kiswahili. Hivyo, ataweza kumtayarisha mwanafunzi wa Gredi ya 3 kutumia Kiswahili sanifu katika mazingira mbatimbali kwa kujithamini na kujiamini.

Compare
Category:
Be the first to review “Moran Stadi za Kiswahili Mwalimu GD3 (Approved) by Kipande”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Reviews

There are no reviews yet.

See It Styled On Instagram

    No access token
Show Buttons
Hide Buttons

Main Menu

1
Scan the code
Thank you for visiting us,

Need any help?