Kamusi ya Semi-Toleo Jipya by Ndalu,Kingei

In stock

by Ndalu, Kingei
Toleo Jipya Ia Kamusi ya Semi ndicho kitabu cha pekee kilichokusanya zaidi ya semi elfu nne. Kitabu hiki kinajumuisha semi, maana yake, pamoja na mifano faafu. Ufafanuzi wa msamiati umetiliwa maanani huku maana kadhaa za semi zikitolewa. Aidha, semi zilizomo humu kitabuni zimepangwa kialfabeti ili kurahisisha urejeleaji. Toleo hili Jipya Ia Kamusi ya Semi ni kitabu kinachowafaa wanafunzi na walimu wa kila daraja: shule za msingi, za upili na hata vyuo vikuu. Hii ni dafina kuu kwa wapenzi wote wa lugha na fasihi ya Kiswahili. Kitula King’ei ni mwalimu, mwandishi, mtafiti na msomi wa lugha na fasihi ya Kiswahili aliye na tajriba kubwa sana. Kwa sasa, ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Ahmed Ndalu amefundisha Kiswahili katika shule za upili na vyuoni, na vile vile kuandika vitabu kadhaa. Hivi sasa, amestaafu kazi ya ufundishaji na anajishughulisha na utafiti na uandishi wa vitabu vinavyoshughulikia nyanja tofauti tofauti za Kiswahili.

Compare
Category:
Be the first to review “Kamusi ya Semi-Toleo Jipya by Ndalu,Kingei”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Reviews

There are no reviews yet.

WhatsApp us for any enquiry...

See It Styled On Instagram

    No access token

Main Menu

Kamusi ya Semi-Toleo Jipya by Ndalu,Kingei

Kamusi ya Semi-Toleo Jipya by Ndalu,Kingei

Select at least 2 products
to compare