-
Made Familiar: Maandazi ya Haiba Level 3
by EMMANUEL
Haiba na marafiki zake wanataka kumnunulia Baraka zawadi anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa. Baraka anaishi na nyanya yake ambaye anaugua. Hata hivyo, kina Haiba hawana pesa. Wanaamua kutafuta njia ya kujitafutia pesa. Je, watafaulu?
-
Made Familiar: Maria taabani
by MWANGI
Maria ana mazoea ya kulala hadi Mama amwamshe. Maria pia husahau kufanya kazi zake za shule hadi Mama amkumbushe. Mama anaenda safari ya mbali. Chacha ambaye ni kakake Maria anataka kumfunza Maria adabu kwa kukosa kumtii. Je, Maria atafanya nini ili
asijipate taabani? -
Made Familiar: Masaibu ya Juma na Bintiheri Level 5
by ATTAS
Mapumziko ya Agosti yanakaribia. Mwalimu Kibahaluli anawaambia wanafunzi wake kuwa wazazi wao wamewaandalia ziara ya kukata na shoka. Ziara hiyo haitakuwa ya kiburudani tu bali pia itawafaa katika kupata majibu ya chemshabongo atakayowapa. Juma, Bintiheri na wanafunzi wenzao wanasubiri likizo ya Agosti kwa hamu na ghamu. Je, Mwalimu Kibahaluli atawapa chemshabongo gani mara hii? Je, safari hiyo itawapeleka wapi?
-
Made Familiar: Mashujaa wa Mazingira Level 5
by OGAL
Mazingira yamejaa aina mbalimbali za taka. Baadhi ya watu wanapata ajali zinazotokana na taka hizi kama vile kukatwa na chupa. Jerry, Tinda na wenzao wanatafuta suluhisho. Je, watafanya nini?
-
Made Familiar: Mbingu Ina Rangi Gani ? Level 1
by JACKSON
Zawadi na marafiki zake wanapenda kutazama mbingu. Wanashangaa jinsi rangi ya mbinguni inavyobadilikabadilika. Je, mbingu ina rangi gani?
-
Made Familiar: Nadia Breaks Her Promise Level 2
by MAGDELINE
Nadia likes attending birthday parties to eat. Jeff, his elder brother, has been invited to a birthday party. Nadia wants to go with him. Jeff complains that Nadia will embarrass him by eating too much. Nadia promises not to eat anything untill Jeff tells her so. Will Nadia keep
the promise? -
Made Familiar: Ndoto za Juma na bintiheri Level 4
by ALI ATTAS
Juma na Bintiheri, ambao ni binamu, wanafunga safari ya Mbuga ya Wanyama ya Tsavo West na Mzima Springs pamoja na wazazi wao. Wanayoshuhudia na kujifunza katika ziara hiyo yanachochea ndoto zao kuhusu kutunza mazingira na kuishi vyema na wanyama wa porini. Pia, yanawafunulia kichemshabongo walichopewa shuleni na mwalimu Kibahaluli. Je, watapata majibu sahihi ya kichemshabongo hicho na kuibuka wanafunzi bora shuleni kwa ubunifu? Jiunge na Juma na Bintiheri katika safari hii ya kiuhalisia na kifantasia iliyojaa vitushi, patashika, mafunzo na vichekesho kwa kusoma hadithi hii ya kusisimua.
-
Made Familiar: Sakata za Juma na Bintiheri Level 5
by ALI ATTAS
Likizo ya Krismasi ilinukia. Zilibaki kama wiki mbili hivi. Mwalimu Kibahaluli alipepeta fikra zake mapema. Alitaka kuwapa kazi za nyumbani wanafunzi wakati wa likizo yao ndefu. Alijua wanafunzi watapumzika vyema likizoni. Vilevile, hakutaka elimu kushika butu.
Alitaka akili zao zibaki angavu. Kwa hiyo, aliwaza na kuwazua kwa muda. Hatimaye kazi ambayo angewapa wakati wa likizo ilimjia ubongoni…
Juma na Bintiheri, ambao ni binamu, pamoja na rafiki yao Lulu wanapofanya utafiti kuhusu kazi waliyopewa shuleni, wanavumbua njia kadhaa za kujipatia mapato. Je, wazazi na walimu wao watakubali na kuwekeza katika uvumbuzi wao?
-
Made Familiar: Siku Yenye Vituko Level 2
by VICTOR
Taji na Furaha wana furaha. Familia yao inaenda safarini pamoja. Je, watashuhudia mambo gani njiani? Jiunge na familia ya kina Taji na Furaha katika safari iliyojaa vituko.
-
Made Familiar: The Broken promise and other stories Level 4
by SABAKAKI
Kibe always find himself between a rock and a hard place. To find his way out, he must apply skills from the subject he fears most—Art and Craft. Kamaria, who loves Art and Craft, often comes to his rescue. For how long will Kibe rely on Kamaria for help?
-
Made Familiar: Tito anatamani Kuchora level 1
by OMONDI
Tito hana vidole mikononi. Hata hivyo, ana ndoto ya kufanya kazi ya kuchora na kupaka rangi kama wazazi wake. Siku moja, mwalimu anawaambia wachore wanyama wapendao. Je, Tito atawezaje kuchora bila vidole? Soma hadithi hii ili ujionee jinsi Tito anavyotumia ubunifu kutekeleza malengo yake.
-
Made Familiar: Unlucky Day Level 1
by Wanyonyi
Niva and Nani wake up to a bright Saturday morning. All seem well until Niva gets chocked, Nani trips on a banana peel and Novel falls on
stairs. Find out how they turn their bad luck to a fun learning experience.
Shop By Categories
- International Curriculum
- Marketplace – Used Books!
- National Curriculum
- TVET/Higher Learning
- Lab Equipment
- General Books
- International Curriculum
- Marketplace – Used Books!
- National Curriculum
- TVET/Higher Learning
- Lab Equipment
- General Books











