-
Shajara yangu ya klabu ya usomaji ya storymoja
Ikiwa unataka kuwa mwerevu zaidi, mjuzi na mwenye kuvutia, soma vitabu vingi zaidi vya hadithi. Ikiwa unapania kuwa mbunifu zaidi ili siku moja uweze kuwa mvumbuzi au mjasiriamali, soma vitabu vingi Zaidi vya hadithi. Ikiwa unataka kazi yenye mapato mazuri na kuchangia katika maendeleo ya taifa katika siku za usoni, soma vitabu vingi zaidi vya hadithi.
Jaza shajara yako kila wakati unaposoma. Onyesha wazazi au mlezi shajara yako na uwaambie kuhusu vitabu ambavyo umevisoma. llinganishe shajara yako na za marafiki zako kisha msherehekee usomaji wenu iwapo mmesoma vitabu vingi. Kusoma kunawezesha! Kusoma ni poa. Kusoma kuna manufaa kwako!
MZAZI: SOMA PAMOJA NA MTOTO WAKO
Furahia uhondo wa kusoma pamoja na mtoto wako. Mtoto wako atavipenda vitabu maishani mwake na atajifundisha kwa wepesi endapo utazingatia hoja kumi rahisi zilizoorodheshwa hapa chini.
1. Soma pamoja na mtoto wako katika mazingira yaliyotulia kama vile kwenye chumba cha kulala.
2. Mhimize mtoto wako awe na mazoea ya kusoma hadithi nzima kwa kutumia viziada vya lugha kama vile kupandisha sauti.Asome hadithi nzima kwanza akilenga kuifurahia tu kisha aisome tena ili ajue yaliyomo. |
3. Mhimize mtoto wako ayaashirie maneno kwa vidole hasa anaposoma hadithi aliyokwisha kuisoma awali.
4. Chunguza kama mtoto wako anaelewa aliyoyasoma kwa kumuuliza maswali kuhusu michoro, wahusika na hadithi mara kadhaa.
5. Kuwa na mtazamo chanya kuhusu hatua anayopiga mtoto wako katika usomaji wake. Usimvunje moyo bali umsifu kwa kila hatua anayopiga.
6. Hakikisha kwamba mtoto wako anaisoma hadithi mara kadhaa.
7. Baada ya mtoto wako kuzoea kusoma hadithi fulani, mhimize ajaribu kukusomea baadhi ya maneno ya hadithi hiyo au hadithi nzima.
8. Mnunulie mtoto wako vitabu tofauti tofauti vya kuburudisha kama vile vitabu vya picha, vya kuchekesha na vya kuelimisha.
9. Mwonyeshe mtoto wako kwamba una nia ya kufuatilia na kujua hadithi anazozisoma kwa kumuuliza maswali kuhusu hadithi hizo. Pia mhadithie hadithi ulizosoma kwenye vitabu ulivyo navyo.
10. Uwe kielelezo bora kwa mtoto wako ili avithamani vitabu. Mwache mtoto wako akuone wewe ukisoma vitabu vingi
-
My First Peak Dictionary fully Illustrated
This dictionary is the only one of its kind for many reasons. In the first place, it is an English-Kiswahili dictionary. Secondly, it has a full-colour illustration for every entry. Third, it targets the early childhood learner as well as the lower primary school pupil. In addition to this, the dictionary focuses on what a child at this Level interacts with on a daily basis. It will surely make a big difference in the learning of both English and Kiswahili at that early age.
-
Mbinu za Kisasa za kufundishia Walimu by Musau
Hakuna kitabu kimoja cha Kiswahili kinachoshughulikia mbinu na mikakati ya kufundisha mada mbalimbali za lugha na fasihi. Mbinu za Kisasa za Kufundishia Kiswahili ni kitabu kinachoshughulikia ufundishaji wa Kiswahili. Kitabu hiki kinabainisha na kufafanua mbinu za kisasa za kufundishia mada kama: matamshi, sarufi, msamiati, ufahamu, insha na fasihi. Dhana muhimu katika ufundishaji wa lugha na fasihi zinafafanuliwa na kutolewa mifano mwafaka inayotokana na tajriba ndefu ya waandishi wa kitabu hiki katika ufundishaji wa Kiswahili. Kitabu hiki kitawafaa walimu wa shule za msingi, za upili na vyuo.
-
Insha Mufti Kioo cha Mwanafunzi by Wallah
Kioo Cha Mwanafunzi
Ufasaha Kamili Ngeli Sahihi Maendelezo Sahihi Msamiati Mwafaka Viambajengo Adhimu Misemo Aali: Tashdidi, Tanakali. Tanakani, Tashbihi, Methali, Nahau n.k. -
Violin Scales and Arpeggios Grade 3
This new edition contains all the scales and arpeggios required for ABRSM’s Grade 3 Violin exam. Includes all Grade 3 scales and arpeggios for the revised syllabus from 2012, with bowing patterns and suggested fingering, along with a helpful introduction including advice on preparing for the exam.
-
Common Mistakes in English by Fitikides
by Fitikides
Common Mistakes in English takes more than 550 examples of typical errors (for example, words that are often confused, misused, or used with the wrong preposition) and offers a correct version and explanation that will help students avoid making the same mistakes themselves. An invaluable book for students who are keen to ‘get it right’ every time. * Offers correct versions and explanations for more than 550 typical errors * Completely updated to reflect modern English usage -
Tenzi Tatu za Kale by MM Mulokozi
by MM Mulokozi
Kitabu hiki ni mkusanyo wa tenzi tatu za kale maarufu: Fumo Liyongo, uliotungwa na Muhamadi Kijumwa; Al Inkishafi, uliotungwa na Sayyid Abdalla bin Ali; na Mwanakupona, uliotungwa na Mwana Kupona binti Mshamu. Kitabu kimehaririwa na M.M. Mulokozi, profesa mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kilichapishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili mwaka 1999.Hizi ni kati ya tenzi maarufu kabisa katika ki-Swahili. Kwa msingi wa sanaa na maudhui, tenzi hizi zina hadhi kamili ya kuwemo katika orodha ambayo kwa ki-Ingereza huitwa “classics.”Fumo Liyongo ni hadithi inayomhusu shujaa Fumo Liongo, ambaye mimi, kutokana na utafiti wangu wa miaka mingi, napendelea kumwita Liongo Fumo. Huyu ni shujaa wa kale, labda miaka elfu moja iliyopita, na ndiye anayesifika kuliko wote tangu zamani katika jamii ya wa-Swahili.Alikuwa pandikizi la mtu, mwenye vipaji kadhaa: kuwashinda maadui, shabaha katika kutumia upinde na mshale, ufundi wa kutunga nyimbo na mashairi. Juu ya yote, alikuwa muungwana sana, mfano wa kuigwa. Lakini alifanyiwa visa na ndugu yake ambaye alikuwa mfalme, hadi hatimaye akauawa na kijana mdogo, ambaye alikuwa mpwa wake.Al Inkishafi ni utenzi wa tafakuri na falsafa kuhusu maisha, ambao umejikita katika kuuliza maana ya maisha ni nini. Mtunzi alilishughulikia suali hili kwa kuzingatia jinsi ustawi na utukufu wa wa-Swahili, hasa wa mji wa Pate, ulivyoanguka. Pate ulikuwa mji maarufu, wenye hadhi na mali, lakini kutokana na masaibu mbali mbali, ullipoteza hadhi hiyo na kuishia kuwa magofu.Hii dhamira imeshughulikiwa tangu zamani na waandishi wengi wa pande za Arabuni, Uajemi, Ulaya na sehemu zingine duniani. Wanafalsafa pia wamehoji maana ya maisha, hasa wanafalsafa wa mkondo wa “existentialism.”Mwana Kupona ni utenzi uliotungwa na mama kumuusia binti yake kuhusu maisha ya ndoa, wajibu wake katika maisha hayo, na wajibu wake kwa watu kwa ujumla. Huu ni utenzi maarufu sana, ambao ni chimbuko la tungo za waandishi wengine, kama vile Shaaban Robert. -
Kamusi Rasmi ya Picha by Yahya Mutuku
by Yahya Mutuku
Kamusi rasmi ya picha imeandikwa kwa upekee usiodhihirika katika kamusi nyingine. Kamusi hii ina sifa zifuatazo- Imeepuka mpangilio wa kialfabeti uliotumiwa na kamusi nyingine. Msamiati umepangwa kwa makundi badala ya kialfabeti kwa sababu wanafunzi katika kiwango hiki bado hawawezi kusaka msamiati kialfabeti (kiabjadi).
- Mkusanyiko wa msamiati unaambatana na ule ulio katika silabasi ya Kiswahili iliyoidhinishwa na taasisi ya elimu nchini (awali Kenya Institute of Education, sasa Kenya Institute of Curriculum Development).
- Kamusi hii ina picha maridadi zinazomvutia mwanafunzi na kumrahisishia kazi.
- Picha zote zimeambatanishwa na maelezo kabambe na kwa lugha nyepesi inayomfaa si mwanafunzi pekee bali mtu yeyote akipendaye Kiswahili.
- Msamiati uliotumika utamwezesha mwanafunzi kujua mengi kwenye mazingira yake.
Shop By Categories
- International Curriculum
- Marketplace – Used Books!
- National Curriculum
- TVET/Higher Learning
- Lab Equipment
- General Books
- International Curriculum
- Marketplace – Used Books!
- National Curriculum
- TVET/Higher Learning
- Lab Equipment
- General Books











