Shingo ya Mbunge na Hadithi Zingine by K.W.Wamitila
by K.W.Wamitila
Shingo ya Mbunge na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko, bulibuli wa hadithi zilizoandikwa na watunzi wanaoonyesha ustadi wa kuumudu utanzu wenyewe pamoja na ukwasi wa lugha ya Kiswahili. Ni mkusanyiko unaotanda mwanda mpana wa kimaudhui kuanzia ukoloni na taathira zake katika jamii hadi siasa ya mfumo wa soko huria. Huu ni mkusanyiko unaoleta pamoja watunzi wa hadithi fupi kutoka Afrika Mashariki, wanaoinukia katika fani na watunzi waliotopea na kubobea katika uga wa utanzu huu. Shingo ya Mbunge na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko aali uliosheheni tashtiti inayokata, ucheshi unaoburudisha na kugutusha na uhondo unaomfanya msomaji kuutamwa ubora wa utanzu huu unaoinukia.
Reviews
There are no reviews yet.