Kamwe si Mbali tena by Said A Mohamed
by Said A Mohamed
“Tambo njoo unisaidie. Nimeshalishika lile jisamaki kubwa linaloogelea huru mawinguni bila ya kumeza ndoana … Leo limemeza ndoana … Njoo unisaidie kulivuta jisamaki hili … Je, sikukwambia, Tambo, kwamba kamwe si mbali tena?”
Katika riwaya hii kila kizazi kinapitia nyakati mbalimbali zinazoathiriwa na usasa. Ina hadithi za watu wanaolishana halua na shubiri. Ndani ya hadithi hizo mnaibuka usuria, utumwa, mapenzi motomoto, wakati wa mporomoko na wakati mpya, ukimbizi wa mtu-kwao, dini ya aina moja inayosimamia dini zote. Wanawake wanakusanya nguvu na hatimaye kukata minyororo. Zaidi ya yote hayo ni miujiza inayooneshwa na wahusika … Haya yote yanasimuliwa na hadithi nyingi katika hadithi moja inayokuzwa na kurambishwa utamu wa lugha.
Reviews
There are no reviews yet.